
BEKI wa Kulia wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari amesaini mkataba wa miaka mwili kuendelea kuitumikia timu ya wananchi Yanga.
Mkataba wa Kibwana ulikuwa unamalizika mwisho wa msimu huu, hivyo kwa mkataba huo ataendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mingine miwili mbele.

Taarifa za kuongezwa kwa kandarasi ya Kibwana Shomari zimethibitishwa na Klabu ya Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.