×

Breaking: Halima Mdee na Wenzake 18 Wafukuzwa Rasmi Chadema – Video

Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa leo kuamkia Alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama.

 

Kabla ya kufikia maamuzi hayo Mwenyekiti wa Chadema taifa aliwapa nafasi ya maridhiano na kuwataka waombe radhi mbele ya baraza kuu ili waweze kusamehewa na wabakie kuwa wanachama. Lakini kwa kauli moja wote walikataa nafasi hiyo na kusema HAWAPO TAYARI KUOMBA RADHI badala yake wanataka maamuzi yafanyike kwa kura.

 

Kufuatia maombi yao ya kutaka maaamuzi yafanyike kwa kura, wajumbe wakapewa nafasi ya kupiga kura ambapo wajumbe 413 wametaka akina Halima WAFURUSHWE, wajumbe 4 wametaka WASAMEHEWE, na wajumbe 6 HAWAFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE.

Matokeo kwa kanda ni kama ifuatavyo;

Kanda ya Victoria
-Wanaokubalia wafukuzwe 42
-Wasiokubali 1
-Wasiofungamana na Upande wowote 1
Jumla kura 44

 

Kanda ya Nyasa
-Wanaokubali wafukuzwe 57
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 57

 

Kanda ya Unguja
-Wanaokubali wafukuzwe 19
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 1
Jumla ya Kura 22

 

Kanda ya Pemba
-Wanaokubali wafukuzwe 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 15

 

Kanda ya Kusini
-Wanaokubali wafukuzwe 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 32

 

Kanda ya Pwani
-Wanaokubali wafukuzwe 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 47

 

Kanda ya Kati
-Wanaokubali wafukuzwe 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 44

 

Kanda ya Serengeti
-Wanaokubali wafukuzwe 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 41

 

Kanda ya Magharibi
-Wanaokubali wafukuzwe 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 37

 

Kanda ya Kaskazini
-Wanaokubali wafukuzwe 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 61

 

Kufuatia maamuzi hayo, wanawake hao 19 si wanachama wa Chadema tena na hivyo wamepoteza rasmi nafasi za ubunge walizokua nazo.

Leave a Comment