×

Biden Asaini Mswada wa Msaada wa Dola Bilioni 40 kwa Nchi ya Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden

RAIS wa Marekani Joe Biden amesaini mswada uliopitishwa na Bunge la Seneti la Marekani wenye thamani ya dola bilioni 40 kwa ajili ya kuisaidia nchi ya Ukraine.

 

Biden amesaini Mswada huo ikiwa ni masaa machache tangu asafiri kwenda Seoul, Korea Kusini ambako yupo katika chakula cha jioni na Rais Mpya wa nchi hiyo.

Joe Biden yupo nchini Korea Kusini kukutana na Rais Mpya wa nchi hiyo

 

Msaada huo unakadiriwa kuwa moja kati ya misaada yenye pesa nyingi ambao Marekani imetoa kwa nchi ya Ukraine lengo likiwa ni kuisaidia nchi hiyo katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini humo.

 

 

Leave a Comment