×

Pablo Aja Kivingine Kuimaliza Geita Gold Leo Jumapili Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba

Wachezaji wa Simba wakifanya yao Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba, amesema watatumia mbinu nyingine kuikabili Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Simba imetoka kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliopita, huku Geita Gold ikishinda 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwa bao la George Mpole aliyefikisha 13.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema: “Tunawajua wapinzani wetu ni imara, hilo halitupi tabu kwani ambacho tunahitaji ni ushindi.

 

“Ngumu kusema mchezo utakuwaje ila ambacho ninajua kwamba tupo tayari kupata ushindi.”

LUNYAMADZO MLYUKA

YAMOTO BAND YAWAKUTA MAZITO, UCHAWI WATAJWA, WENYEWE WAFUNGUKA | DSM FLAVOUR

Leave a Comment