
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto leo Mei 26, 2022 amemwomba Rais Uhuru Kenyatta msamaha baada ya wawili hao kutofautiana pindi tu baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa 2018.
Tofauti kati ya Rais Kenyatta na naibu wake zimekuwa wazi ambapo rais haungi mkono azma ya Ruto ya kuwania urais katika uchaguzi wa Agosti na badala yake anamuunga mkono kinara wa upinzani Raila Odinga.
Wakati wa mkutano wa kila mwaka wa maombi ya Alhamisi ulioandaliwa na bunge, Ruto alimwomba rais msamaha.
“Pia najua kuwa kuhudumu kama naibu wa rais huenda sikufikia matarajio ya bosi wangu Rais Kenyatta na ninaomba unisamehe,” alisema.
Aliendelea kumtakia rais kustaafu kwa amani ambapo Kenyatta anamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho mwaka huu.
Rais hana mamlaka ya kumtimua naibu wake – anaweza kuondolewa tu madarakani iwapo atapigiwa kura bungeni au kutokuwa na uwezo.