Rais Samia Akutana na Kufanya Mazungumzo na Rais wa Ghana Nana-Akufo Addo
Global Publishers May 26, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Ghana Nana Akufo-Addo kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ya Accra (Jubilee House) nchini Ghana.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ghana Nana-Akufo Addo, Ikulu Accra nchini Ghana.
Rais Samia yupo nchini Ghana kwenye ziara yake ya ikazi ya siku tatu (3) ambako alifanikiwa kukabidhiwa tuzo yake ya Babacar Ndiaye Tuzo inayotolewa kwa Rais ambaye amekuwa mjenzi bora wa miundombinu wa mwaka barani Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo katika Ikulu ya Accra (Jubilee House) nchini Ghana tarehe.