×

Kocha Pablo Afunguka Hali ya Kikosi cha Simba Kuelekea Kuwakabili Yanga CCM Kirumba

Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco Martin

KOCHA Mkuu wa Simba Sc, Pablo Franco amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, Mchezo utakaopigwa kesho Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Pablo amesema morali ya wachezaji ipo juu na wanaonekana wanahitaji kujitoa kwa ajili ya kupata ushindi katika mchezo huo muhimu kwao msimu huu.

Pablo amesema tangu timu yake ilivyocheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Geita Gold kikosi kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.

Pablo amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea pambano la kesho dhidi ya Yanga

“Jambo zuri ni kuwa wachezaji wapo katika hali nzuri, morali ipo juu na wanafanya vizuri mazoezini. Tunahitaji kushinda mchezo wa Jumamosi ingawa tunajua utakuwa mgumu,” amesema Pablo.

Kuhusu wachezaji majeruhi Pablo amesema wote wanaendelea vizuri na matumaini ya kuwatumia kwenye mchezo wa Jumamosi ni makubwa.

Leave a Comment