×

Chongolo Awaasa Wananchi Shinyanga Kutunza Miundombinu ya Maji

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiongea na wananchi wa Kata ya Mwakitojo mkoani Shinyanga

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo amewasihi wananchi hasa wanao jihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini kutunza miundombinu ya maji ambayo Serikali imeweka kwenye maeneo yao ili iwasaidie kuepuka adha ya ukosefu wa maji safi.

 

Chongolo ameyasema hayo wakati anaongea na wananchi katika Kata ya Mwakitojo mkoani Shinyanga ambapo amekagua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya milioni 324 mradi ambao unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100.

Mradi wa Maji unaojengwa mkoani Shinyanga katika Kata ya Mwakitojo

Mradi huo unatarajiwa kuwasaidia wananchi zaidi ya 14600 wanaoishi katika eneo hilo ambao shughuli yao kubwa ya kiuchumi ni uchimbaji wa madini.

 

Chongolo anaendelea na ziara yake ya siku 7 katika Mkoa wa Shinyanga yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali lakini pia kufanya shughuli za chama ndani ya Mkoa huo.

 

Leave a Comment