
DAR ES ALAAM, Jumatano Juni 2022: Airtel Tanzania leo imetangaza TESA KIMILIONEA INAENDELEAAAA ambapo kwa sasa wateja na mawakala watakuwa wanajishindia zaidi.
TESA KIMILIONEA ZAIDI itatoa Tsh milioni 1 kila siku huku zawadi kubwa ikiwa ni kujishindia Tsh milioni kumi na gari mpya aina ya Toyota RAV4 mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni nyongeza ya muda wa promosheni kwa mwezi mmoja zaidi.

Awali, promosheni ya TESA KIMILIONEA ilikuwa inawapa fursa Watanzania 100 kushinda laki moja kila siku, wateja na mawakala wawili kushinda milioni moja kila wiki huku zawadi kubwa ya milioni 10 au zawadi ya gari aina ya Toyota IST moja kwenye droo kubwa kila mwisho wa mwezi kwa kufanya miamala mbalimbali na mara kwa mara.

Wateja na mawakala watahitajika kutumia moja ya huduma hizi ili kuingia kwenye droo ya TESA ZAIDI KIMILIONEA: Kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money, kufanya miamala ya kibenki, huduma za kutuma pesa nje ya nchi, kununua bando na kununua muda wa maongezi, na kwa mawakala kuweka na kutoa pesa kupata fursa hii, wateja watahitajika kupiga *150*60#na kufanya miamala au kufanya miamala kupitia Applikesheni ya Airtel.
Akizungumza jijini Dar leo wakati wa kutangaza TESA KIMILIONEA INAENDELEA Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda alisema;

Promosheni hii ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ni moja ya uthibitisho wa jinsi tunavyorudisha kwa wateja wetu ili kuongeza hamasa katika kutumia huduma zetu za fedha kwa mtandao wa Airtel Money kwa matumizi mbalimbali. Nawatakia kila la kheri wateja wetu wote.
“Kupitia malengo yetu ya muda mrefu tumekuwa tukiwekeza kwenye upanuzi wa mtandao kwa kuongeza idadi ya maduka yetu ya Airtel Money, Branches pamoja na mawakala na vilevile kuzindua matumizi ya applikesheni na kuendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa mtandao pamoja na ubunifu wa huduma zetu. Tunaendelea kuwapatia wateja wetu huduma zilizo bora zaidi.”
Kwa upande wa Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema;
Airtel tumedhamiria kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia promosheni hii ya TESA KIMILIONEA kila mteja au wakala wa Airtel Money anayo fursa ya kushinda hivyo niwaombe kuendelea kutumia huduma za Airtel Money kwani ndiyo njia pekee ya kuingia kwenye droo na hivyo na kuwa mshindi”.
Baada ya kusema hayo sasa tuwatafute washindi wa droo kubwa ya mwezi uliopita yupo atakayejishindia gari aina ya Toyota IST na mwingine atajishindia milioni 10 wote hawa walitumia huduma yetu ya Airtel Money kwa mwezi uliopita wa promosheni ya TESA KIMILIONEA
Katika promosheni hiyo washindi walipatikana na taratibu za kuwakabidhi zawadi zao ulikuwa ukiendelea.