
VILABU vya Simba na Yanga vimesaini Mkataba na Kampuni ya Agrinfo iliyojikita katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao kwa pamoja wamezindua kampeni maalum ya Nani Zaidi wenye lengo la kuviwezesha vilabu hivi vikongwe nchini Tanzania kuboresha uchumi wao.
Akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo mzima wa utekelezwaji wa zoezi hilo muwakilishi kutoka Azam PAY, Bwana Mziray amesema zoezi hilo litakuwa la uwazi na wanachama na wapenzi wa vilabu hivyo vikongwe nchini watapata fursa ya kupiga kura zao kwa kutumia mitandao ya simu za Vodacom kwa njia ya M-Pesa, Tigo kwa njia ya Tigopesa pamoja na Airtel kwa njia ya Airtel Money.
Akiongea na waandishi wa habari CEO wa Simba Barbara Gonzalez amesema zoezi hili limekuja katika wakati mzuri kutokana na majadiliao ya pande zote kwa maana Simba, yaga pamoja na washirika wengine kama Azam Pay, Azam Media pamoja na Makampuni ya simu.

“Kwenye Commercial interests za vilabu lazima tuwe pamoja, mwezi wan ne tulianza mchakato, mwezi wa Tano tukasaini Mkataba tukasema ngoja tukae kimya mpaka tumalize mchakato mzima, leo ni mwezi wa sita tumekamilisha jambo ambalo kwa Simba hii ni Phase Two (Awamu ya Pili) kutoka ile kampeni ya Tumeamua Tunaweza.” Alisema Barbara.
Naye CEO wa Yanga Senzo Mbata amesema hii ni fursa adhimu ambayo kama vilabu hawawezi wakaipoteza na ni kwa mara ya kwanza imetokea nchini Tanzania ambapo vilabu hasimu vimekaa kwa pamoja na kuangalia namna muhimu ya kukuza vipato vyao na kuhakikisha vilabu vyao licha ya upinzania uliopo lakini vinapata mafanikio Zaidi na Zaidi.
Wakati huohuo Senzo amesisitiza kuwa kampeni hiyo haihusiani kabisa na kampeni ya mabadiliko ambayo klabu ya Yanga inendelea kutekelza ambayo inahusisha wananchama kujiandikisha kwa kulipia shilingi 29,000 kama ada ya uanachama kwa mwaka mzima.