
KATIBU MKUU wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amezitaka Mamlaka zinazohusika na uhifadhi wa wanyamapori kuwavuna viboko ambao wamekuwa wakivamia mashamba na nyumba za wananchi katika Wilaya ya Busega wakitoka ndani ya Ziwa Victoria kutokana na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo vya wananchi.
Chongolo ametoa kauli hiyo leo Wilayani Busega ikiwa ni siku yake ya mwisho ya ziara yake ya siku nne mkoani Simiyu, ambapo akiwa katika Wilaya amepokea malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi juu ya kusumbuliwa na wanyama hao mara kwa mara.
Wananchi hao wamemweleza Katibu Mkuu huyo kuwa kwa sasa wameacha kulima, kutokana na vikobo kuwa wengi sana ambapo makundi makubwa ya viboko kila siku yamekuwa yakivamia makazi yao pamoja na mashamba.

Wilaya hiyo ambayo eneo lake kubwa linapakana na Ziwa Victoria, ambapo Katibu Mkuu Chongolo ameeleza kuwa kama wanyama hao wamekuwa wengi kuna haja ya kuwavuna ili wasiendelee kuleta madhara kwa wananchi.
Amesema kuwa suala hilo atalipeleka kwa Mamlaka husika na kuwashauri wavune wanyama hao, au kutafuta njia nyingine ya kuweza kupambana nao ili wasilete madhara kwa wananchi na kuharibu mazao yao.
“ Nitakwenda niwaambie wahusika kama viboko wamezidi sana waje wawavune,