×

Yanga Yapania Kufanya Makubwa Kimataifa, Yaanza Harakati za Usajili

Kikosi cha Yanga kimekuwa na msimu mzuri ktika mashindano ya ndani ya Ligi Kuu ya NBC na Kombe la FA

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umeelezea mikakati yake kuelekea msimu ujao kuwa ni kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa wanayotarajia kushiriki kutokana na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22.

Yanga inahitaji pointi tatu ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu, lakini pia imetinga Fainali ya Kombe la FA na endapo itabeba taji hilo itakuwa na nafasi nyingine ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hersi Said Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Hersi Said ameeleza kuwa moja ya mikakati yao ni kuzidi kukiboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa wa michuano hiyo, jambo ambalo anaamini litawasaidia kufikia malengo yao.

“Ukweli hiki ambacho wamekiona msimu huu ni kidogo, msimu ujao tumepania kufanya kufuru zaidi kwenye usajili tayari kuna wachezaji tuponao kwenye mazungumzo na wengine wameshasaini mikataba ya awali na uzuri usajili wetu una baraka za wakuu wetu wa benchi la ufundi kwa hiyo mashabiki watulie,” anasema Hersi.

Hersi amesema kuwa kwa hatua ambayo Yanga imefikia wachezaji ndio wanalilia kutaka kusajiliwa na siyo wao kumbembeleza mchezaji, lakini hiyo imetokana na mafanikio na ubora ambao timu hiyo imeuonesha msimu huu wa ligi.

sifaelpaul

Leave a Comment