
MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongela amethibitisha kuuawa kwa askari wa Jeshi la Polisi baada ya kupigwa mshale katika eneo la Loliondo wakati akiendelea kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na usalama.
Aidha John Mongela amethibitisha kuwepo kwa amani ya kutosha na kuwataka wanaosambaza taarifa za uongo mitandaoni waaache mara moja.
RC Mongela amesema kumekuwa na upotoshwaji wa makusudi wa kutumia baadhi ya picha ambazo nyingi ni za miaka mitatu au minne iliyopita.

Wakati huohuo RC Mongela amebainisha kuwa mbali na kifo hico hakuna majeruhi mwingine yeyote yule kwenye hospitali zote za Mkoa wa Arusha anayehusika na tukio la Loliondo.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai kama kuna mwananchi yeyote aliyejeruhiwa na vyombo vya ulinzi na usalama basi ajitokeze apewe huduma kwani Serikali ya awamu ya 6 ni Serikali sikivu na inaendeshwa kwa utawala wa sheria na demokrasia.