×

Rais Samia Alilia Usawa wa Kibiashara Baina ya Oman na Tanzania(PICHA+VIDEO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongea kwenye kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania nchini Oman

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuna kila haja ya kuwa na mbinu mbadala juu ya usawa wa kibiashara kati ya Nchi ya Oman na Tanzania.

 

Rais Samia ameyasema hayo akiwa nchini Oman kwenye ziara yake ya kikazi akiwa katika Kongamano la wafanyabiashara wa Oman na Tanzania.

 

Rais Samia amesema kuwa inabidi jitihada za makusudi zifanyike ili kuona namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika zaidi katika biashara baina ya mataifa hayo mawili kwani anaamini Tanzania inaweza kusafirisha bidhaa nyingi kwenda nchini Oman zaidi ya kiwango kinachosafirishwa kwa sasa.

 

Kwa upande mwingine Rais Samia amebainisha kuwa katika sekta ya uwekezaji Tanzania imefanikiwa kukua zaidi ya Oman kwani hadi kufikia mwezi Aprili 2022, Tanzania imeweza kuwekeza katika miradi 62 ambayo yamegharimu jumla ya kiasi cha Dola Milioni 308.35 na kufanikiwa kutengeneza nafasi 2489 za ajira katika Nyanja za Kilimo, Rasilimali watu, Uzalishaji wa rasilimali, Mawsiliano, Miundombinu pamoja na Utalii.

Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania wakimsikiliza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Akiongea kwenye kongamano hilo Rais Samia amesema anatambua kuwa kumekuwa na sheria na sera mbalimbali ambazo zinabana mazingira amzuri ya ushirikiano wa kibiashara lakini yeye kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amebainisha kuwa atasimamia kuona sera na sheria hizo zinafanyiwa marekebisho ili ziweze kuleta manufaa na mazingira mazuri ya ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo.

 

Rais Samia ametoa rai wa wafanyabiashara wa nchini Oman kuangalia fursa zilizopo Tanzania na kuja kuwekeza kama ambavyo Tanzania itaangalia nini cha kufanya katika nchi ya Oman.

Leave a Comment