×

Vodacom Yashinda Tuzo Nne kwa Mpigo na Kuwa Kampuni Bora

Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (katikati) akipokea tuzo ya Innovative Telco Company of the year 2021 toka kwa Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya ambapo Vodacom walishinda tuzo hiyo kutokana na uwekezaji wake na uboreshaji wa mtandao na huduma bora kuzidi makampuni mengine ya mawasiliano kwenye tuzo za Tanzania Digital Awards zilizoandaliwa na Serengeti Bytes. Kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare. 

 

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania Plc, Harriet Lwakatare akionesha tuzo ya Best Customer Care Telco Company iliyotolewa na Taasisi ya Serengeti Bytes kupitia tuzo zake za Tanzania Digital Awards, ambapo Vodacom Tanzania walishinda tuzo hiyo kutokana na huduma bora za kidigitali kwa wateja, huduma hizo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni hiyo, Kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando na Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya.

 

 

Kaimu mkuu wa idara ya Uhusiano na mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Christina Murimi (katikati) akipokea tuzo ya Telco company of the year 2021 toka kwa Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya ambapo Vodacom walishinda tuzo hiyo kutokana na uwekezaji wake na uboreshaji wa mtandao na huduma bora kuzidi makampuni mengine ya mawasiliano kwenye tuzo za Tanzania Digital Awards zilizoandaliwa na Serengeti Bytes. Kushoto ni Meneja wa Chaneli za kidijitali na malipo kwa mtandao wa M-Pesa, Josephine Mushi.

Leave a Comment