
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza Serikali kubadili utaratibu uliopo ili kuwakopesha magari watumishi wa umma wenye hadhi ya kuwa na gari la Serikali ikiwa ni mkakati wa kubana na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima.
Amesema kuwa utaratibu huo alioupendekeza utasaitia kuokoa gharama za matumizi ya magari kwa zaidi ya Sh500 bilioni.
Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.
“Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza Wizara, napendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita”amesema
HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI KUU KWA MWAKA 2022-23
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx