×

Waziri wa Biashara, Zanzibar Akutana na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO

Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (WIPO).

LEO tarehe 14 Juni 2022, Mhe. Omar Shaaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar ambaye ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 12 wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Daren Tang, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (WIPO).

Picha ya pamoja ya Waziri Omar pamoja na Watendaji wengine akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa WIPO

Waziri amemshukuru Mkurugenzi Mkuu huyo kwa miradi na programu zilizotekelezwa na shirika hilo nchini.

 

Kwa upande wake Bw. Tang ameahidi kutekeleza miradi/programu zaidi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo ya kilimo, ubunifu, kuandaa sera ya Haki Miliki, kuwajengea uwezo wajasiliamali vijana na wanawake.

 

Aidha, ameahidi kuwajengea uwezo wataalam wanaosimamia masuala ya Hakimiliki na Mahakama ya Biashara.

Leave a Comment