
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa ameingia Bungeni akiwa pamoja na Timu ya Taifa ya Walemavu Tembo Worriors baada ya kukaribishwa Bungeni na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Akson ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Juni 16, 2022 Dodoma kwa ajili ya kupongezwa baada ya Kufuzu Kumbe la Dunia litakalochezwa nchini India.

