×

Bosi Mpya wa Chelsea Awatahadharisha Mashabiki Wasitarajie Usajili Mkubwa

Bosi mpya wa Chelsea Toddy Boehly

BOSI na Mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea Todd Boehly amewaonya mashabiki wa Klabu ya Chelsea kuwa wasitarajie usajili mkubwa katika majira haya ya kiangazi kutokana na kuwepo kwa sheria ya Financial Fair Play (FFP) ambayo inatishia mustakabali wa biashara yake.

 

Bosi huyo ambaye tangu akabidhiwe rasmi timu hiyo, klabu sasa imeruhusiwa rasmi kuanza kusajili tena baada ya kuwa kwenye kizuizi tangu Mmiliki wa zamani wa klabu hiyo Mrusi Roman Abramovich kukumbwa na vikwazo kutoka kwa Serikali ya Uingereza.

 

Hadi sasa klabu hiyo haijafanikiwa kukamilisha usajili wowote ule huku ikiendelea kuhusishwa na golikipa kinda wa klabu ya Chicago Fire ya nchini Marekani Gabriel Slonina.

 

Nyota wengine ambao wanahusishwa na klabu hiyo ni pamoja na Ousmane Dembele ambaye anamaliza mkataba wake na klabu ya FC Barcelona, Jules Kounde beki wa kati wa klabu ya Sevilla na Timu ya Taifa ya Ufaransa pamoja na winga wa Manchester City Raheem Sterling.

Beki wa kati wa klabu ya Sevilla na Timu ya Taifa ya Ufaransa Jules Kounde

Lakini pia kuna baadhi ya maeneo mengine muhimu ambayo mashabiki wa klabu hiyo wanatamani kuona yakifanyiwa kazi lakini Boehly ameonya akisema kuwa kuna mambo mengine muhimu ambayo klabu lazima iyafanye.

Sheria ya Financial Fair Play imeanza kuwa na meno kwa sasa na hiyo itazuia uwezo wa kusajili wachezaji kwa kiasi chochote kile cha pesa. Uefa inalichukulia jambo hili kwa umakini mkubwa na itaendelea kufanya hivyo.” Alisema Boehly akiiambia Bloomberg.

Winga wa Barcelona Ousmane Dembele

Kiasi cha dola milioni 200 kinatarajiwa kutolewa kwa kocha Thomas Tuchel kusajili wachezaji katika majira haya ya joto pamoja na kiasi kingine amabcho kinaweza kutokana na mauzo ya wachezaji.

Leave a Comment