
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewaasa wakandarasi wazawa kutumia vema na kwa ufanisi fursa wanazopewa na serikali za ujenzi wa miradi mbalimbali ili kuendelea kupewa nafasi hizo zaidi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati aliposimama na kukagua ujenzi wa daraja la Nyeburu linalounganisha eneo la Pugu na Chanika Jijini Dar es salaam ambalo ujenzi wake umekuwa ukisuasua.

Makamu wa Rais ameonesha kutofurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo ambapo amaesema ujenzi wa daraja hilo umechukua muda mrefu na kutoa athari kwa wananchi hasa wakati wa mvua licha ya serikali kuendelea kutoa malipo kwa wakati kwa mkandarasi katika kila kazi.