
CHAMA cha Mawakala wa Bima Nchini (IAAT) leo Juni 23,2022 leo kimefungua mkutano wake mkuu wa tatu ambapo walikuwa wakijadili changamoto zao mbalimbali ndani Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Kamishna wa Bima nchini, Hadija Saidi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na mawakala kutoka nchini nzima ulianza kwa risala iliyosomwa kwa mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Bima nchini (IAAT) Sayi John. Risala hiyo ilielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili na kumuomba mgeni rasmi afikishe vilio hivyo kwa serikalini ili ziweze kutatuliwa kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Miongoni mwa changamoto walizomueleza mgeni rasmi ni pamoja na mawakala wenzao wa Zanzibar kutojiunga na umoja wao wa wa IAAT hivyo kushindwa kupigania haki zao kwa pamoja. Mwenyekiti huyo amesema lingine linalolalamikiwa sana na wanachama wake ni kucheleweshewa kamisheni zao na makampuni ya bima wanayofanya nayo kazi.

Baada ya risala hiyo baadhi ya mawakala nao walipewa nafasi ya kutoa maoni yao kwa mgeni rasmi na kumuomba ayafikishe serikalini ili yafanyiwe kazi. Mmoja wa mawakala hao kutoa mkoani Mwanza amemwambia mgeni rasmi kuwa kuna umuhimu wa kuweka sheria ya kampuni za bima kuingia mikataba maalum na mawakala wao ili kudhibiti mambo mbalimbali ikiwemo ucheleweshewaji wa kamisheni zao.

Akijibu risala na maoni ya mawakala hao, Naibu Kamishna Hadija alianza kuwapongeza mawakala hao kwa kuandaa mkutano huo wa kujadili mambo yao mbalimbali ikiwemo kubadilisha uzoefu kwa mawakala wapya na wazoefu. Naibu Kamishna Hadija amewaambia mawakala hao kuwa amepokea changamoto zao na kuwaahidi kuziwakilisha serikalini kwaajili ya kuzitatua.

Akijibu maswali ya wanahabari kuhusu wanaopatwa na majanga kucheleweshewa malipo ya fidia zao, Naibu Kamishna Hadija amesema hilo kwasasa halipo labda mdai fidia mwenyewe acheleweshe kukamilisha vielelezo kama vile taarifa za polisi na vielelezo vingine. Ameendelea kusema Naibu Kamishna Hadija kuwa wengine wanaona usumbufu kufuatilia vielelezo na kujikuta wakiishia njiani na kulilaumu shirika la bima.

Akiendelea kuzungumza kamishna huyo amewaonya mawakala wote wa bima nchini kujisajili chama cha makala wa bima nchini IAAT na kusisitiza kuwa hilo ni lazima na atakayekiuka atachuliwa hatua za kisheria. Mkutano huo unaendelea tena kesho Ijumaa Juni 24 ukumbini hapo.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/GPL