×

Gavana wa Ukraine Atoa Amri Majeshi ya Nchi Hiyo Kuondoka Severodonetsk

Gavana wa Luhanski Serhiy Haidai

GAVANA wa Jimbo la Luhansk Serhiy Haidai amesema majeshi ya Ukraine hayana budi kutimka katika eneo la Severodonetsk kutokana na eneo kubwa la Jimbo hilo kushikiliwa na majeshi ya Urusi.

 

Ingawa Gavana huyo hajabainisha wazi ni lini vikosi hivyo vitaondoka lakini amesisitiza hakuna sababu ya vikosi hivyo kubaki katika eneo ambalo kwa asilimia kubwa lieshikiliwa na vikosi vya Urusi.

Vikosi vya Ukraine vikiwa katika misafara ya kijeshi

“Maeneo yaliyokuwa yamesalia yamesambaratishwa vipande vipande kwa miezi kadhaa sasa, hivyo hakuna sababu ya msingi yoyote ile ya kuendelea kukaa katika maeneo hayo.” alisema Serhiy.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uingereza siku ya alhamisi ilibainisha kuwa wanajeshi wa Ukraine walilazimika kukimbia maeneo ya Severodonetsk na Lysychansky kwa kuogopa kuzungukwa na majeshi ya Urusi.

Serhiy Haidai Gavana wa Luhansk nchini Ukraine

Kama Urusi itafanikiwa kukamata miji ya Severodonetsk na Lysychansky itakuwa imefanikiwa kukamata miji mikubwa miwili ambayo inaunda Mkoa wa Luhansk ambao ni moja kati ya mikoa miwili inayounda Donbas.

 

Leave a Comment