
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo katika utaratibu wake wa kawaida wa kukutana na Vyama vya Siasa Nchini tarehe 28 Juni, 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amekuwa akitekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa mapema wakati anaingia madarakani ya kutaka kuwa na siasa safi na shirikishi kwa Vyama vyote vya Siasa nchini kuhakikisha anasaidia navyo katika kuleta maendeleo ya kweli ndani ya nchi