
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Tuma Abdallah kuwa Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)
Mbali na Tuma, wengine walioteuliwa ni Mhandisi Bashiri Juma Mrindoko kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO). Mrindoko ni Katibu Mkuu Mstaafu.
Pia amemteua Profesa Shaban Athuman Chamshama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF). Chamshama ni Prof. wa Saynasi ya Misitu na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.
Aidha, Rais Samia amemteua Sarah Kinyamfura Barahomoka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprises Limited (PRIDE). Barahomoka ni Mwandishi Mkuu wa Sheria Mstaafu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wengine walioteuliwa ni Thams Shangwe amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfumko wa Self Microfinace (self -MF). Shangwe ni Mkurugenzi wa Sera na Utaratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. Dk Oswald Jotam Masebo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa (NMT). Dk Masebo ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Profesa Emmanuel Amaniel Mjema ametuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Mjema ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam.
