
KLABU ya Azam FC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu.
Edinho anajiunga na Azam FC akitokea klabu ya ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.

Nyota huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.
Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao.
Tape Edinho anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC baada ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior kutoka klabu ya Sol FC ya kwao.