
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mariam Mwinyi wamejumuika na Viongozi mbalimbali katika hafla ya chakula cha jioni walichoandaliwa na mwenyeji wao Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na Mkewe Angeline Ndayubaha Ndayishimiye, Ikulu Bujumbura.

Rais Dk. Mwinyi yupo nchini Burundi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi zitakazofanyika Julai 1, 2022.