
KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania imekamilisha usajili wa wachezaji Andreas Christensen beki wa kati aliyemaliza mkataba wake akiwa na klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza pamoja na Franck Kessie aliyemaliza muda wake akiwa na klabu ya AC Milan ya nchini Italia.
Wachezaji wote hao walikuwa huru ambapo wote walisaini mikataba ya awali tangu mwezi januari mwaka huu walisubiri tu kutamatika kwa msimu na kutambulishwa rasmi kama wachezaji wapya wa Blaugrana.

Sambamba na usajili huo Barcelona pia wanaangalia uwezekano wa kukamilisha dili la kumsajili winga wa Leeds United Raphinha ambaye pia anawaniwa kwa karibu na klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.
Tayari wachezaji wa Barcelona wameanza kuripoti kambini kwa ajili ya kujiandaa na maadalizi ya msimu mpya wa 2022/2023 chini ya kocha Xavi Hernandez.