×

Man United Yakamilisha Dili la Malacia, Yahamishia Nguvu kwa De Jong wa Barcelona

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag akiwa na Tyrell Malacia baada ya kusaini mkataba wa miaka minne (4)

KLABU ya Manchester United imekamilisha dili la kumsajili mlinzi kutoka klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi Tyrell Malacia kwa ada ya paundi milioni 12.9 ambayo inatarajiwa kupanda hadi kufikia paundi milioni 14.6 kwa kipindi cha miaka mine (4) huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

 

Malacia alikuwa akigombaniwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya vikiwemo Totenham Hotspurs.

Tyrell Malacia (22) Mchezaji mpya wa Manchester United

Malacia mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kuwa pendekezo la kocha mkuu wa klabua hiyo Erik Ten Hag ambaye amemfutailia kwa karibu tangu akiwa nchini Uholanzi.

 

Malacia anachangia wakala HCM Sports Management pamoja na kiungo raia wa Uholanzi Frenkie De Jong wa Barcelona ambaye naye anatajwa kukaribia kujiunga na mashetani wekundu wa Old Trafford

 

 

Leave a Comment