×

Mkutano Mkuu Wamuidhinisha Injinia Hersi Kuwa Rais Mpya wa Yanga kwa Miaka Minne Ijayo

Mkutano mkuu wa klabu ya Yanga umeidhinisha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Eng Hersi Said kuwa Rais mpya wa klabu kwa miaka minne ijayo.

Hersi aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, amepitishwa rasmi na mkutano mkuu maalum wa uchaguzi unaoendelea muda huu kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa katiba ya TFF, Mgombea wa nafasi yoyote akiwa mmoja kwenye kugombea nafasi hiyo Wajumbe hupiga kura za NDIYO na HAPANA ambapo Mgombea anapopata kura nyingi za NDIYO basi moja kwa moja anakuwa ameshinda.

Leave a Comment