×

Yanga Ijayo Mtakoma Kiungo wa Newcastle Aaga Burundi Tayari Kutua Jangwani

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Newcastle ya England ambaye anatarajiwa kutua kwa mabingwa wa Tanzania Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Newcastle ya England ambaye hivi sasa anaichezea Glentoran ya Ireland, Gael Bigirimana, tayari ameaga kwao Burundi.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Mgombea wa Urais wa Yanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa timu hiyo, Injinia Hersi Said kumtangaza nyota huyo.

 

Mshambuliaji huyo muda wowote atatambulishwa na Yanga mara baada ya kufikia makubaliano mazuri ya usajili.

 

Yanga imepania kushusha mashine za maana kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, na tayari imeshawatambulisha Lazarous Kambole na Bernard Morrison huku Bigirimana na Aziz Ki wakitarajiwa kufuata.

 

Bigirimana juzi katika ukurasa wake wa Instagram, aliwaaga mashabiki wa timu yake anayoichzea hivi sasa ya Glentoran akisema anakwenda kwenye changamoto mpya.

Kiungo huyo muda wowote atatua nchini kwa ajili ya utambulisho, mara baada ya kufikia muafaka mzuri na kusaini mkataba.

 

Gael kwa kupitia mtandao wa Instagram, aliandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki.

“Ninafurahia na nipo tayari kwa changamoto ijayo,” aliandika kisha akaweka alama ya imoji ya mtu anayeshukuru.

 

“Nataka kusema asante kubwa kwa mashabiki wote, uongozi na wachezaji wenzangu @glentoranfootballclub (timu ya Glentoran).

 

“Ninafurahia sapoti yote mliyonipa kwa kipindi cha miaka miwili! Nawatakia kila lakheri katika msimu ujao.”

STORI: WILBERT MOLANDI, IBRAHIM
MUSSA NA MUSA MATEJA

Leave a Comment