Makamu wa Rais Awapa Vodacom Tuzo Tatu Maonesho ya 46 ya Sabasaba Dar
Global Publishers July 13, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa katika shangwe la ushindi. KATIKA kuhitimisha maonyesho ya biashara ya 46, Vodacom Tanzania imeibuka tena kuwa mshindi wa jumla kwenye mawasiliano. Hii ni kutokana na muendelezo wa uwekezaji kwenye mitambo, huduma kabambe za kibunifu na rasilimali watu. Huduma mbalimbali kwenye nyanja za afya, elimu, kilimo, huduma za kifedha, bima, burudani na huduma kedekede za kidijitali. Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini. Pamoja tunaweza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Phillip Mpango (kulia) akimkabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa sekta ya mawasiliano Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania Plc Nguvu Kamando, baada ya kampuni hiyo kuibuka kidedea katika maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yaliyomalizika.