
MSHEREHESHAJI Maarufu nchini MC Gara B leo Julai 14, 2022 ametembelea Studio za Global TV na Global Radio ambapo amefanya mahojiano huku akigusia kwa upekee ishu ya tukio la uchumba kati ya Harmonize na Kajala.

Gara B amesema kumekuwa na maneno kuwa yeye ndiye aliyehusika kwa namna moja au nyingine kumshawishi Kajala kurudiana na Harmonize lakini amebainisha kuwa hiyo si sahihi ingawa alifanya jitihada za kuhakikisha anamshawishi Kajala ili arudiane na Harmonize lakini jitihada zake ziligonga mwamba kutokana na Kajala kumzungusha.

“Kwanza kipindi ambacho kimeumana mimi nilipigiwa simu, nilivutiwa waya na kuambiwa bro eeh kwa heshima uliyonayo you can do something the way unavyoheshimiwa hata kwa Kajala hebu tafadhari fanya kitu kwa maan ahiyo nilihusishwa kwa namna moja ama nyingine kwenye kuweka mambo sawa kitu ambacho pia hakikuwa rahisi kwa sababu tayari K mwenyewe alikuwa kama amesha Move on, nikimpigia simu hivi apokee kweli anapokea tunakubaliana kuwa tukutane hivi tuyajenge lakini ikifika time anakupa Excuse.” Alisema MC Gara B

Aidha mshereheshaji huyo mwenye wafuasi wengi mitandaoni amegusia ishu ya sherehe ya nyota wawili wa muziki wa Bongo Fleva kati ya Billnass na Nandy ambapo amewapongeza kwa ujasiri wa kushikamana pamoja licha ya changamoto walizopitia pamoja ambazo watanzania wengi wanazitambua.