×

Abiria 41 Wanasurika Kifo Baada ya Basi la Happy Nation Kugongana Uso kwa Uso na Lori

Muonekano wa gari la Happy Nation baada ya kugongana uso kwa uso na Lori

ABIRIA 41 waliokuwa wakisafiri na basi la Happy Nation wakitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza, wamenusurika katika ajali baada ya basi lao kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo ni uzembe wa dereva wa basi aliyeacha njia yake na kulifuata lori hilo.

Leave a Comment