
MHESHIMIWA Jumaa Aweso (Mb)-Waziri wa Maji New Delhi nchini India amekutana na kuzungumza na Ms. Harsha Bangari, Mkurugenzi Mtendaji wa India Exim Bank.
Katika kikao hicho Mheshimiwa Aweso kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishukuru Benki Exim India kwa kushirikiana na Tanzania hususani Sekta ya Maji katika kutekeleza Miradi Mbalimbali ya Maji ikiwemo Mradi mkubwa wa Maji wa Shinyanga-Igunda Tabora na Tinde-Shelui.
Aidha, amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa India Exim Bank kwa kuendelea na ufadhili katika utekelezaji Mradi wa kihistoria wa Miji 28 ambapo Benki hiyo imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 500.
Katika hatua Nyingine, Waziri Aweso ameiomba Exim Bank India kuendelea kushirikiana na kuiunga mkono Tanzania kifedha katika muendelezo wa kutekeleza miradi ya Maji ya kimkakati na kutoa wasilisho lenye mapendekezo ya maeneo muhimu kwasasa huku akilenga na kusisitiza kwa pamoja kuendelea kudumisha mashirikiano baina ya Tanzania na India eneo muhimu la Maji.

Katika hatua nyingine kwenye kikao hicho ni agenda muhimu ya ombi la Mhe.Waziri kwa India Exim Bank kwa umuhimu na katika kikidhi dhamira na nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassaan kuwezesha upatikanaji wa Fedha kwa Tanzania katika katika kufanikisha MJI WA DODOMA kutekeleza Mradi wa kutoa Maji Ziwa Victoria ambapo eneo hili lina changamoto kubwa ya Maji kutokana na ongezeko la watu na Mradi wa RUFIJI-DAR ES SALAAM ikiwa ni Kuelekea hatua kubwa ya kumaliza Changamoto ya Maji katika Majiji hayo.