×

Chelsea Mbioni Kukamilisha Usajili wa Beki Mbadala wa Christensen

Jules Kounde Beki wa Sevilla

KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza ipo mbioni kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa klabu ya Sevilla ya nchini Hispania raia wa Ufaransa Jules Kounde.

 

Taarifa zinadai kuwa mara baada ya ofa yao ya awali ya Euro milioni 42 kukataliwa Chelsea ilirudi na ofa mpya ya Euro milioni 55 ambayo inakaribia kabisa kiwango cha pesa kilichokuwa kinahitajika na klabu hiyo ili kuinasa saini ya Kounde.

Jules Kounde (23) raia wa Ufaransa

Kounde (23) amekuwa moja ya changua la muda mrefu la Kocha wa Klabu hiy Mjerumani Thomas Tuchel ambaye alimfungia kazi majira ya dirisha dogo la msimu uliopita lakini hakufanikiwa kuinasa saini yake.

Tajiri na Mmiliki wa Chelsea Todd Boehly

Kumekuwa na taarifa kuwa klabu ya Barcelona nayo ipo katika vita ya kupigania kuinasa saini ya nyota huyo huku tayari kukiwa na makubaliano bifasi baina ya mchezaji na klabu ingawa hadi sasa kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Barca bado hawajatuma ofa rasmi kwa klabu ya Sevilla.

Leave a Comment