×

Asasi za Kiraia Zapewa Elimu Juu ya Masuala ya Kujitolea, Kutoa Msaada kwa Jamii

Shirika la Foundation of Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na  East Africa Philanthropy Network (EAPN) wamewakutanisha asasi za kiraia kwa lengo la kuwapa elimu, kuchochea na kutoa hamasa juu ya masuala ya kujitolea na kusaidia jamii.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Philanthropy Network, Evans Okinyi amesema kongamano hilo pia limetoa elimu na hamasa juu ya namna za kutumia nguvu za wananchi katika rasilimali za ndani na utandawazi.
Aidha Okinyi aliziomba asasi zote zilizohudhuriaji kufanya mambo makuu matatu amvayo ni kuzalisha
maarifa juu ya kutumia nguvu za jamii za ndani ya nchi, kujitolea na kutoa msaada mbalimbali kwa wenye uhitaji.
“Tunatakiwa kuwa na ushirikiano na wananchi na kuhakikisha tunaiweka jamii mbele, piia tuutumie majukwaa kama EAPN kuonyesha kazi zinazo fanyika katija kusaidia jamii zetu,” amesema Okinyi
Naye mmoja wa wazungumzaji katika kongamano,Ofisa Mkuu wa Maudhui Kampuni  ya PZG Impact Communications Firm, Prudence Glorious alisisitiza juu ya nguvu ya mawasiliano katika kufikisha madhumuni ya asasi hizo kwenye kusaidia jamii kupitia vyombo vya habari vya kuchapisha, televisheni na mitandao ya kijamii.
Alielezea, “Unapowasilisha madhumuni yako ya kusadia jamii inahitaji kuwa na simulizi lenye kugusa hisia. Ni rahisi watu kuguswa kihisia na simulizi kwani ndivyo tunavyojenga uaminifu na mahusiano.” amesema Glorious na kuongeza
“Fahamu changamoto unazoshughulikia na tofauti ambayo shirika lako linaleta kwa idadi na data. Unaweza kuzitoa idadi hizo wakati unapowasiliana na wadau wanaoweza kukusaidia rasilimali kwa ajili ya shughuli zako za kutoa misaada,” amesema
Katika kongamano hilo, zaidi ya waleta mabadiliko 50 wa mashirika ya kiraia walihudhuria, miongoni mwao alikuwepo Rose Nzali kutoka IOGT-NTO Movement EA ambaye aliguswa na mawasilisho ya nguvu ya utoaji na shuhuda juu ya athari iliyonayo hivyi kuchukua hatua ya kuichangia taasisi ya Doris Mollel Foundation.
Aidha Rose aliwahimiza washiriki wengine waliohudhuria kuichangia taasisi hiyo. Mwishoni mwa Kongamano hilo, Karin Rupia kutoka FCS, alishauri waliohudhuria kongamano hilo kujitokeza na kushughulikia masuala yanayohitaji msaada katika jamii kwa kutumia zana ambazo tayari watu wanamiliki.
Pia aliwasihi wahudhuriaji kujumuisha wanafamilia na marafiki zao katika harakati za kutoa misaada.
“Kusema kwamba unafanya uhisani, kujitolea au uchangiaji sio tu kuhusu kutoa rasilimali za kifedha bali ni kutoa nguvu na uwezo wako pia  kwasababu aina yoyote ya juhudi ndogo zinazowekwa katika kutoa msaada huleta mabadiliko makubwa,” amesema

Leave a Comment