×

Poulsen Asikitishwa Taifa Stars Kunyimwa Fursa ya Kuutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Kim Poulsen

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen amesikitishwa na kitendo cha Mamlaka za soka kuinyima ruhusa timu hiyo ya Taifa kupata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

Poulsen amebainisha kuwa anajisikia vibaya na anshindwa kuelewa dhana ya kuinyima timu ya taifa faida ya kufanya mazoezi na maadalizi ya mechi kwenye nyasi halisi za Uwanja wa Mkapa na badala yake wanapelekwa kwenye nyasi za bandia ilihali mchezo dhidi ya Somalia utachezwa katika Uwanja wenye nyasi halisi wa Benjamin Mkapa.

 

Amesisitiza kuwa kitendo cha Taifa Stars kunyimwa fursa angalau siku moja kabla ya mechi hiyo huku mashindano ya U-20 yakipewa kipaumbele kuliko Taifa ni jambo linaloshangaza.

Poulsen ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha Taifa Stars kunyimwa nafasi ya kuutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa

“Nashangaa na kiukweli nashindwa kuelewa, kwamba tunapokuwa Taifa Stars tunacheza mchezo wa kufuzu Fainali za CHAN, mchezo muhimu na haturuhusiwi kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa!”

 

Aidha Kocha Poulsen amebainisha kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri isipokuwa beki wa kushoto David Luhendeambaye anamsumbuliwa na maumivu ya misuli ambaye amethibitisha kuwa hatahusika kabisa kwenye mchezo huo wa kesho.

Stars inatarajiwa kucheza na Somalia kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya mtoano dhidi ya Somalia ambapo atakayeibuka mshindi atacheza dhidi ya Uganda ili kupata mshindi atakayefuzu kushiriki fainali za CHAN.

Leave a Comment