×

Rais Samia Agusia Uwekezaji Kwenye Sekta Usafiri wa Anga kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Kenya Uhuru Kenyatta wakizindua rasmi ujenzi wa barabara ya Afrika Mashariki yenye urefu wa kilomita 42.4

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amegusia kuwepo kwa mchakato wa uwekezaji katika sekta ya usafirishaji wa anga kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Rais Samia ameyasema hayo katika Mkutano hafla ya uzinduzi wa barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4 Ngaramtoni Arusha leo Julai 22, 2022.

Rais Samia akihutubia halaiki iliyojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Barabara ya Afrika Mashariki

“Lakini si hayo tu tunajitahidi sana pia kuongeza usafiri wa anga ili biashara ya usafiri na usafirishaji wa watu uweze kufanyika kwa kiwango kikubwa ndani ya Afrika Mashariki nan je ya Afrika Mashariki na hivyo kukuza biashara ndani ya ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.” Amesema Rais Samia.

Rais Samia akiwa pamoja na Rais Kenyatta

Aidha Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wanaoishi kwenye maeneo yote ambayo miradi hiyo inapita kutumia fursa hizo kujinyenyua kiuchumi na kuimarisha zaidi sekta za utalii, sekta za kilimo na sekta nyingine za biashara ili kuchangia zaidi kwenye ukuaji wa uchumi wa taifa na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wakizindua rasmi Barabara ya Afrika Mashariki

Pia Rais Samia amewaasa watanzania kushirkiana kwa pamoja kutunza miundombinu kwani miradi hiyo imetumia gharama kubwa katika utekelezaji wake.

Leave a Comment