
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameomba radhi kwa jumuiya za jamii za wenyeji nchini Canada, kutokana na mateso waliyoyapata, yaliyosababishwa na kanisa hilo.
Papa Francis, ameyasema hayo jana Jumatatu katika Mji wa Maskwacis, Alberta katika ziara yake nchini Canada.

Ameeleza kuwa, sera za kanisa hilo kuanzia miaka ya 1880 hadi miaka ya 1970, kanisa hilo liliwatenganisha kutoka kwenye familia zao na kuwalazisha kujiunga na shule zilizokuwa zinaendeshwa na kanisa hilo.
Wakiwa katika shule hizo za kidini, watoto wengi walipitia mateso ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.
“Kwa unyenyekevu mkubwa, naomba radhi kwa niaba ya kanisa kwa jamii za wenyeji wa Canada kwa dhambi kubwa iliyofanywa na Wakatoliki wengi kwa wenyeji,” amenukuliwa.