
WATU milioni moja katika Jimbo la Wuhan nchini China, ambapo kirusi cha Covid 19 kiligunduliwa kwa mara ya kwanza Mwaka 2020, wafungiwa kutoka nje baada ya kugundulika visa vinne.
Wakazi wa Wilaya ya Jiangxia, wameamuriwa kukaa ndani ya Nyumba zao kwa siku tatu baada ya kupatikana kesi nne za Covid, Kwa sasa hivi China inafuata mkakati wa “Covid Sifuri” pamoja na upimaji wa watu wengi, huku sheria za watu kukaa ndani zikiwa zinaendelea kuzingatiwa.

Hatua hiyo imepunguza idadi ya vifo kuliko katika nchi nyingine nyingi, lakini mkakati huo unakabiliwa na upinzani kutoka kwa wafanyabiashara ambao wanaendelea kukabiliwa na vikwazo.
Wuhan ni Jiji lenye watu takribani milioni 12, upimaji wa kawaida ulifunua kesi mbili katika siku mbili zilizopita, Kesi nyingine mbili zilipatikana muda mfupi baada ya agizo la kufuli kutolewa.

Wuhan ilijulikana Ulimwenguni kote, mapema mwaka 2020 kama mahali pa kwanza Wanasayansi kugundua Kirusi cha Corona, na kuwa Jiji la kwaza kuwekwa chini ya hatua kali za vizuizi.
Pia nchi nyingine zilifuata kuchukua hatua hiyo lakini baadae China ilijulikana kama hadithi ya mafanikio ya Covid, na vizuizi viliondolewa mapema zaidi kuliko katika nchi nyingine nyingi Duniani.