×

Kidunda, Katompa Kitaumana Kesho Uwanja wa Majimaji Mjini Songea

Mabondia Seleman Kidunda na Tshimanga Katompa kuzichapa kesho Uwanja wa Majimaji, Songea

MABONDIA Seleman Kidunda na Tshimanga Katompa wamepima uzito tayari kwa kesho Jumamosi kupanda ulingoni kuwania ubingwa WBF Intercontinental Afrika katika pambano litakalopigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Majimaji mijini hapa.

 

Mabondia hao wamepima uzito jana kwenye stendi ya daladala iliopo mjini hapa tayari kwa pambano hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu sambamba na Karim Mandonga anayetarajia kupanda ulingoni dhidi ya Shabani Kaoneka ambao watacheza pambano la utangulizi.

Tayari mabondia wote wameshapima uzito kwa ajili ya kupanda ulingoni kesho Julai 30, 2022

Kidunda na Katompa watapanda ulingoni katika pambano hilo ambalo litapigwa kwa raundi kumi kwenye uzani wa Super middle.

 

Pambano hilo limedhaminiwa na Global TV Online na Gazeti la Championi.

Leave a Comment