
MSOMAJI wa magazeti ya Global Publishers na mfuatiliaji wa vipindi vya +255 Global Radio na Global Tv, Anna Muro Njau, wa Lugalo Dar, usiku wa jana Alhamisi alisherehekea Send Off yake na kuzua shangwe kubwa wakati akimtambulisha mumewe mtarajiwa Fred Mathew Mabula.

Sherehe hiyo ilifanyika Ukumbi wa Golden View uliopo Mbezi Beach Tangi Bovu jijini Dar ambapo ilinogeshwa na wageni waalikwa waliopendeza kupitiliza.

Katika pati hiyo ya kihistoria katika maisha yake Anna alipata nafasi ya kukata keki, kula, kunywa na kucheza na wageni waalikwa wakiwemo wazazi wake.

Sherehe ikiwa imenoga ulifikia muda wa kumtambulisha mumewe mtarajiwa ndipo alipoenda kumuinua mkaka mtanashati aliyenyooka vizuri akiwa amependezeshwa na suti ya kisasa na kuonekana ‘smati’ kama walinzi wa rais.

Anna alimtambulisha kijana huyo kwa jina la Fred Mathew Mabula kitendo kilichozua shangwe na nderemo kutoka kwa wageni waalikwa ukumbini humo.
Akizungumza na Global Tv, Anna alisema anamshukuru sana mwenyezi mungu kwa siku hiyo ya kihistoria kwake ya kujiandaa kuelekea kwa mumewe mtarajiwa ambaye ni zaidi ya rafiki kwake.

“Yaani furaha niliyonayo kwangu haielezeki chamsingi hapa tuombe uzima kuelekea kwenye ndoa yetu inayotarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 30 mwaka huu.