×
Global Publishers
  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Hadithi
    • Mikasa
    • Siasa
  1. Home
  2. Habari
  3. Waziri Mkenda: RUWASA Ijitathmini Inamhujumu Waziri Aweso Usimamizi wa Maji Rombo

Waziri Mkenda: RUWASA Ijitathmini Inamhujumu Waziri Aweso Usimamizi wa Maji Rombo

Global Publishers July 29, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umetakiwa kujitathmini kutokana na kadhia ya kushindwa kusimamia mradi wa maji Wilayani Rombo.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prf Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo tarehe 26 Julai 2022 wakati akiwa katika muendelezo wa ziara jimboni humo ambapo amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa Bilioni 2.9
Prof Mkenda amekagua mradi huo ambao mkandarasi alisaini kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka huu 2022 lakini mpaka sasa hakuna kazi iliyokwisha kufanyika zaidi ya kuwekwa mchanga na kokoto zisizozidi hata gari moja.
Prof Mkenda amesema kuwa ameamua kufika na kukagua chanzo cha maji katika mto Wona ambapo mradi huo utakapokamilika utarahisisha upatikanaji maji kwa lita Milioni 4 kwa siku na kupunguza kwa kiasi kikuwa tatizo la maji Rombo linaloikabili Wilaya ya Rombo.
“Tatizo namba moja, mbili, na tatu Rombo ni maji sasa mtu anayechezea mradi wa maji sielewi ana madhumuni gani na anataka wananchi wa Rombo wawe na taswira gani kwa serikali, wanamhujumu Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso ambaye ni mchapakazi na kwa hili nitamualika aje aone changamoto hii” Amekaririwa Prof Mkenda
Amesema kuwa Mradi huo ni sehemu ya miradi ya maji yenye jumla ya Bilioni 10 iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maji Wilayani Rombo.
“Kwa kuwa sehemu hiyo ni ngumu kufika sio rahisi kwa viongozi kufika na kuona maendeleo ya mradi huo inakuwa rahisi kuficha mapungufu haya kwahiyo RUWASA inabidi ijiangalie upya kwa kuwa ndio msimamizi wa mradi huo” Amesisitiza Prof Mkenda
Mhe Prof Adolf Mkenda ambaye ni mbunge wa Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro amesema kuwa kwa sasa katika Wilaya ya Rombo, RUWASA inatia shaka usimamizi wake wa miradi ya maji hvyo amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo kutembelea Rombo ili kujionea kadhia hiyo ya ucheleweshwaji wa mradi wa maji.
Na Mathias Canal, Rombo
SHARE THIS:
Previous Next

Related Posts

Mastaa Wa Yanga, Max, Skudu Na Nkane Walivyonogesha Uzinduzi wa Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya NIC - Global Publishers HABARI

Mastaa Wa Yanga, Max, Skudu Na Nkane Walivyonogesha Uzinduzi wa Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya NIC

October 17, 2023
Mwigulu Aivaa TFF, Simba Kutolewa Ligi ya Mabingwa - Global Publishers HABARI

Mwigulu Aivaa TFF, Simba Kutolewa Ligi ya Mabingwa

June 22, 2021
Airtel yazindua ‘HATUPIMI Bando’ - Global Publishers HABARI

Airtel yazindua ‘HATUPIMI Bando’

March 21, 2017
Mkutano wa Trump, Putin Alaska Waisha Bila Makubaliano ya Kusitisha Mapigano Ukraine – Video - Global Publishers HABARI

Mkutano wa Trump, Putin Alaska Waisha Bila Makubaliano ya Kusitisha Mapigano Ukraine – Video

August 16, 2025

Leave a Comment Cancel reply

You must be logged in to post a comment.



DAKTARI

GLOBAL TV Online




SIMBA
YANGA
NEWS
Global Publishers
  • About Us
Download on the App Store
Get it on Google Play

© 2026 Global Publishers. All Rights Reserved.

Designed by Yatosha Web Services