×

Chelsea Kumnasa Cristiano Ronaldo, Wachambuzi Wadai Kwa Sasa Hastahili Kuchezea Man United

Cristiano Ronaldo, Mshambuliaji wa Manchester United

KLABU ya Chelsea wametakiwa kufanya kila wawezalo ili kumnasa Cristiano Ronaldo katika usajili mkubwa, wakati anataka kuondoka Manchester United au Mashetani Wekundu.

Baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku, Chelsea haijafanikiwa kusaini Mshambuliaji mwingine

“Cristiano Ronaldo yuko kwenye timu maskini sana, Man United walikuwa maskini sana msimu uliopita na bado alifunga mabao 18 ya Premier League,” anasema beki wa zamani wa Chelsea au The Blues, Scott Minto katika Kipindi cha White and Jordan kwenye Mtandao wa talkSPORT.

Kocha wa chelsea Thomas Tuchel

“Unaweza kubishana kwamba yote yanamhusu yeye (Ronaldo), lakini bado unaweza kukaa naye chini na kusema; ‘Tazama tunakuhitaji ufanye hivi, je, uko tayari kufanya hivyo? Ikiwa sivyo hatutakuja kwa ajili yako. Ikiwa ni wewe, tutafanya…” anamalizia Minto na kuongeza;

“Ana uwezo wa kushinikiza -siyo kwamba hawezi kuifanya, ni kwamba hataki kuifanya.”

 

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment