
DIWANI wa Viti Maalum jiji la Dar es Salaam, Beatrice Nyamisango jana aliungana na wanawake wanaharakati wenzake walipokuwa wakisherehekea Siku ya Mwanamke wa Afrika ambapo Kauli mbiu yao ilikuwa ni Umuhimu wa Mwanamke katika Sayansi.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Human Diginity Foundation (HUDEFO) chini ya Mwanzilishi wake Sara Pima, Shirika la Kimataifa la UNESCO na wadau wengine ilifanyika Jengo la Tanzanite jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Beatrice na wageni wengine walipata nafasi ya kujadiliana mambo mbalimbali yaliyokuwa yakilenga kumkomboa mwanamke na kumuwezesha kwenye somo la sayansi.

Waheshimiwa wengine waliohudhulia hafla hiyo ni pamoja na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation, Wanu Hafidh, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga Mwanaisha Ulenge na wengineo.