×

Sistiinho: Simba Day, Wiki ya Wananchi na Azam Festival ni Faida Kwa Timu na Jamii

Sistiinho, mchambuzi wa soka

MCHAMBUZI wa soka kupitia vipindi vya michezo vya Global tv online na +255 Global Radio, Sistiinho amebainisha kuwa Simba Day, Wiki ya wananchi na tamasha la Azam zinafaida kuu mbili kwa jamii na timu hizo.

 

Amesema kuwa kipindi hiki jamii inapaswa kunufaika na uhusiano uliopo kati ya wachezaji pamoja na jamii ambayo kimsingi hiki ndiyo huwa kipindi rasmi kabla ya kuanza kwa hekaheka za msimu mpya wa 2022/2023.

 

Koffi Olomide alitumbuiza katika kilele cha wiki ya wananchi msimu uliopita

“Kwanza ni mpira kurudi kwa jamii kupitia mashabiki wa timu hizo kufanya mambo mbalimbali yanayogusa jamii kama kutembelea vituo vya yatima, wasiojiweza na wagonjwa pia kutoa damu mahospitalini na kufanya shughuli za maendeleo kama usafi na ujenzi.” amesema Sistiinho.

Marioo alitumbuiza tamasha la Simba SC

Aidha ni wiki ambayo timu hizo kupitia mashabiki wake kuingiza kipato kikubwa kwenye mauzo ya jezi mpya zinazozinduliwa na mauzo ya tiketi na bidhaa zingine za siku hizo kwahiyo kunakua na “fan engagement” kubwa sana”

Leave a Comment