×

Rais Samia Azindua Mradi wa Maji Makongorosi Wilayani Chunya, Agusia Kuhusu Barabara

 

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua Mradi wa Maji, Makongorosi Chunya

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi wa maji katika eneo la Makongorosi lililopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

 

Rais Samia amezindua mardi huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayoendelea Mkoani Mbeya ambapo amepata fursa ya kutembelea na kuzindua baadhi ya miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Rais Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi wa Makongorosi Chunya

Akiongea na wananchi wa Makongorosi Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutia nguvu katika kuhakikisha inasogeza huduma za kijamii kwa wananchi lakini pia amewaomba wananchi waendelee kukiamini Chama Tawala Chama cha Mapinduzi katika kuendelea kuongoza dola nchini Tanzania.

 

Aidha Rais Samia akiwa katika ziara yake hiyo amegusia suala la barabara ambapo amebainisha kuwa barabara iliyojengwa imeigharimu Serikali zaidi ya kiasi cha Shilingi Bilioni 67, pesa mbazo akama zingetumika kwenye sekta ya Afya au Elimu basi ingekuwa na tija kubwa zaidi.

Leave a Comment