×

Ndege Yalipuka Wakati Ikitua Jijini California, Rubani na Abiria Wanusurika

 

 

Ndege iliyodondoka

RUBANI pamoja na abiria waliokuwa kwenye ndege ndogo yenye injini moja wamenusurika kifo baada ya ndege hiyo kulipuka wakati ikielekea kutua katika Uwanja wa ndege Jijini California nchini Marekani.

 

Andrew Cho ndiye aliyekuwa Rubani wa ndege hiypo na baada ya kuona ndege inaanza kumshinda akaamua kutua katikati ya magari kwenye barabara ya 91 Freeway iliyopo Corona mashariki mwa Los Angeles lakini katika hali ya kushangaza yeye pamoja na abiria wake wote walitoka wakiwa salama kabisa.

 

Utuaji wake ulikuwa wa kutisha ambapo bawa moja la ndege liligonga gari lililokuwa linapita barabaranihali iliyosababisha ndege kukata kona na hatimaye kulipuka kabla ya rubani na abiria kuepuka moto uliolipuka.

 

 

 

Rubani na abiria wote wamenusurika na kifo

“Ulikuwa ni kama mshindo mzito hivi, ngumu kuelezea.” Cho aliiambia KTLA.

Tulikuwa hatua kama nne au tano hivi kutua, ndipo ndege iligoma jumla na ikadondoka chini.

 

Aliendelea kwa kusema kuwa ni kutokana na mafunzo aliyopewa ndiyo yaliyosababisha hadi akafanikiwa kutua na ndege hiyo chini.

 

 

 

 

 

 

Leave a Comment