×

Mwili wa Aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi Kenya Aliyetoweka Waokotwa

Daniel Musyoka

ALIYEKUWA Msimamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) katika Jimbo la Embakasi Mashariki, Daniel Musyoka amekutwa amefariki na mwili wake kuonekana katika eneo la Kajiado nchini humo.

 

Musyoka alitoweka katika eneo lake la kazi Agosti 9, 2022 ikiwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya

Aidha taarifa iliyotolewa na Maafisa wa Polisi katika eneo hilo ilibainisha kuwepo kwa mwili wa mwanaume majira ya jioni ya Agosti 15 huku taarifa zaidi zikieleza kuwa mwili wa huo ulionesha kuwa na majeraha yaliyotokana na mapambano.

 

Tayari Uchaguzi nchini Kenya umemalizika kwa Rais Mteule William Ruto kutangazwa mshindi kufuatia uchaguzi Mkuu ulioanza Agosti 9, 2022

Leave a Comment