
Viongozi mbali mbali wa kimataifa wameendelea kutuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto kufuatia kutangazwa kwake Jumatatu kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 9 Agosti.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema:’’ Ninawapongezaa Wakenya kwa uchaguzi wao mkuu wa amani na kutangazwa kwa Dr William Ruto kama Rais mteule. Tunatazamia kuendelea kufanya kazi na makaka na madada zetu nchini Kenya kuimarisha uhusiano wetu wa karibu. Tuko pamoja’’:
I congratulate the people of Kenya on their peaceful general election and the subsequent announcement of Dr @WilliamsRuto as President-elect. We look forward to continue working together with our brothers and sisters in Kenya to strengthen our historically close ties. Tuko pamoja
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) August 16, 2022
Katika ujumbe wake wa Twitter Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema ”ningependa kumpongeza rais mteule wa Kenya William Ruto na watu wa Jamuhuri ya Kenya kwa kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wa amani.”
My heartfelt congratulations to the President-elect @WilliamsRuto and the people of the Republic of Kenya for holding free, fair and peaceful elections. We urge all the parties to preserve peace, and disputes be resolved by existing competent legal mechanisms. Idumu jumuiya yetu!
— SE Evariste Ndayishimiye (@GeneralNeva) August 15, 2022
Naye Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari amesema ningependa kuwapongeza watu wa Kenya kwa uchaguzi wa amani, na matokeo yenye uwazi, ambayo kwa mara nyingine tena yanaonyesha kuwa mchakato wa demokrasia ,maadili na kanuni vinasalia kuwa njia bora kwa watu kwa kuwachagua viongozi wao na kuwawajibisha
I congratulate the President-Elect of Kenya, William Ruto, on his victory in the August 9, 2022 general elections. I wish him a successful inauguration and tenure in office, while also looking forward to more fruitful and robust engagements between Nigeria and Kenya.
— Muhammadu Buhari (@MBuhari) August 15, 2022